Mwenge wa Uhuru 2024 umepokelewa leo Septemba 25, 2024 Wilayani Kyerwa ambapo umepitia jumla ya miradi ya maendeleo sita kwa kufungua miradi 2, kuitembelea miradi 2, kuweka jiwe la msingi mradi1, kuzindua mradi 1, na kufungua mradi 1. Miradi hiyo ya maendeleo ina thamani ya shilingi Bilioni 8.5
Miradi ambayo imetembelewa na mwenge wa uhuru 2024 ni ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitahitaji maalum katika Shule ya Sekondari Mabira, ujenzi wa kiwanda cha kukoboa kahawa cha Kaderes-Kitwe, ujenzi wa barabara ya lami ya Rubwera Sekondari KM 1 iliyopo Rwenkorongo Kyerwa, ujenzi wa wodi ya magonjwa mchanganyiko katika kituo cha Afya Nkwenda,ujenzi wa mradi wa maji wa Karongo Rwabwere na mradi wa Kikundi cha Bodaboda ni Ajira Kashanda katika Viwanja vya Standi ya Nkwenda.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava, akizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kutembelea na kukagua miradi hiyo, amesema miradi yote ambayo imepitiwa na mwenge imetekelezwa kwa kiwango kinachoridhisha pia aliwapongeza wasimamizi wa miradi hiyo huku akiwaasa wananchi na wasiamamizi kuitunza hiyo na kuiendeleza ili iweze kutoa huduma zilizokusudiwa kwa wananchi wa Wilaya ya Kyerwa.
Aidha, ndungu Mzava amefungua bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum ambalo limegharimu shilingi milioni 165,000,000 ambalo lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi wa kiume 80 ambao wanasoma katika shule ya sekondari Mabira huku akifanya matendo ya huruma kwa kuwazawadia vifaa saidizi wanafunzi hao wenye mahitaji maalum.
Ndugu Mzava amempongeza Mwekezaji anayejenga kiwanda cha kukoboa kahawa cha Kaderes Kitwe ambacho kinajengwa na mwekezaji wa ndani Ndugu Leonard Kachebonaho na kusema kuwa kitatoa ajira kwa wananchi na kupunguza shughuli za magendo ambayo huchochewa na bai ndogo ya kahawa hivyo kiwanda hicho kitakuwa suluhisho la magendo kwa kuongeza thamani ya zao la kahawa.
Ndugu Mnzava akizungumza katika Kijiji cha Nyakatuntu baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi ametoa wito kwa viongozi na wadau mbalimbali kutumia nafasi zao na kufanya mikutano na wananchi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya uchaguzi utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024 nchini na kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na taarifa sahihi juu ya uchaguzi huo.
Aidha, ameipongeza Halmaahauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa kutenga fedha za mapato ya ndani kuwezesha ujenzi wa wodi ya wanaume magonjwa mchanganiko iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 230,000,000 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao utatoa huduma kwa wananchi na kusaidia ustawi wa jamii na amezitaka taasisi zote za Umma kufanya manunuzi yote katika mfumo wa NeST.
Vile vile Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru ametembelea barabara na kuzindua mradi wa maji pamoja na kutembelea mradi wa Vijana Bodaboda ni Ajira Kashanda huku akipokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa ujumbe wa bio za Mwenge wa Uhuru 2024.
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukabidhiwa kukesha katika eneo la standi ya Kwenda na Kukabidhiwa Mapema kesho Novemba 26, 2024 katika Shule ya Msingi Kyaka-Kyaka kwaajili ya kukimbizwa katika Wilaya ya Missenyi
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved