Mtandao wa wafugaji Nkwenda UNKWERWAKI, umepata fursa ya mafunzo ya siku moja juu ya ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa toka taasisi ya Animal Breeding East Africa (ABEA).Mafunzo haya yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa UNKWERWAKI hapa Nkwenda.
Katika mafunzo haya yaliyoendeshwa na Mr.Gidi na Fransis toka ABEA, wafugaji walifundishwa jinsi ya kumjua mnyama jike anapokuwa katika joto kwa ajili ya upandishaji,vyakula vifaavyo kumlisha mnyama ili atoe maziwa kwa wingi, jinsi ya kupima uzito wa mnyama, aina za ng’ombe wa maziwa , na suala la uhamilishaji kwa ujumla.
Aidha, wataalam hao walimtambulisha ndugu Baraka Rutenge kama mhamilishaji wa Wilaya ya Kyerwa ambaye atapatiwa vifaa vya uhamilishaji na kuanza kazi hiyo mwezi Juni, 2018.Jumla ya wafugaji therathini walishiriki, wanawake 24 , na wanaume 6.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved