Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe ametembelea Kata ya Bugara kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za Wananchi zinazowakabili katika maeneo yao na zikihitaji serikali kuzishughulikia.
Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo amewaasa wazazi hasa akinababa ambao huuza mashamba bila ya ridhaa yafamilia nzima na baadae kutelekeza familia zao na kukosa mahitaji muhimu ikiwemo chakula.
“Baba kwenda kuingia mkataba wa kuuza shamba ambalo linatumika kwa ajili ya mazao ya chakula ya nyumbani iwapo mama hajaridhia wala famila yake haijaridhia, akinamama jifungeni kanga msikubali… iko sheria ya kukulinda msikubali.” Ameeleza Mhe. Msofe.
Mhe. Msofe amewashukuru TANAPA kwa kuyaondoa makundi ya tembo yaliyokuwa yanavamia maeneo ya wananchi na kupelekea madhara kwa wanadamu na mazao yao na kuwataka wajipange kutoa mafunzo kwa vijana ili wajue namna ya kukabiliana na tembo pindi watakaporudi katika maeneo hayo.
Vile vile ametoa maelekezo kwa wanaodai fidia iliyosababishwa na madhara ya tembo kuvamia maeneo yao wafike katika ofisi za wahusika ili waweze kuchukuliwa taarifa zao na kuona namna ya kuwalipa fidia zao.
Pia kero za barabara mbovu na makaravati yasiyopitika muda wote, kutokuwa na Vitambulisho vya taifa, migogoro ya ardhi, pamoja malalamoiko ya mapato ya Mnara wa simu ni miongoni mwa kero zilizojitokeza na kutolewa ufafanuzi na wataalam walioambatana na Mkuu wa Wilaya huku kero zingine zikichukuliwa kwa ajili ya utekelezaji zaidi.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved