Mradi wa sambaza mbegu fasta katika Wilaya ya Kyerwa ulianzishwa mwezi mei, 2017 na ulitekelezwa kwa ufanisi katika Vijiji vinne vya Nyabishenge,Nyabikurungo,Rwenkende na Masheshe.
Katika kikao cha mrejesho wa mradi huu uliomaliza muda wake julai, 2018 ,mtaalam toka kituo cha utafiti cha Ukiriguru ndugu Beka Chilimbi( aliyemuwakilisha Mtendaji Mkuu wa taasisi ya utafiti Ukiriguru) alishukuru Wilaya ya Kyerwa kwa ushirikiano mzuri waliotoa wananchi kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi ambapo lengo la kaya kuongeza lishe,kipato na uhakika wa chakula kupitia viazi lishe limefanikiwa.
Aidha, naye Afisa Kilimo na ushirika wa Wilaya ndugu Meshack Libent alitoa takwimu za uzalishaji wa mbegu 1,805,000 zilizalishwa ambapo tani 4.03 za viazi zilipatikana.Idadi ya wakulima waliopewa mbegu bure kutoka katika mashamba ya Vijiji vyote vinne ni 870.
Akihitimisha kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ndugu Shadrack Mhagama aliwashukuru wafadhiri wa mradi huukwa mambo makuu mawili.Moja ni ongezeko la uzalishaji wa viazi vitamu na mbegu zake(pingili), na pili ni elimu iliyopatikana kwa kipidi cha utekelezaji kwamba itabadili utamaduni wetu wa ulaji na matumizi ya viazi vitamu.
Mwisho aliahidi kuhakikisha mbegu hizi zinasambaa katika shule ili watoto wanufaike na uji na chakula wawapo masomoni.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved