Mradi wa kuimarisha mifumo ya sekta za Umma (Public Sector Strengthening System-PS3) umeendesha mafunzo ya mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa katika vituo vya kutolea huduma ujulikanao kwa kitaalam kama "FFARS".Akifungua mafunzo hayo ya siku mbili(2) yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Bernard iliyopo Rubwera,kata ya Kyerwa Wilayani Kyerwa, mgeni rasmi ndugu Nassoro A. Ngurungu aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, aliwasisitiza wajumbe kuwa makini katika kipindi chote cha mafunzo ili thamani ya fedha inayopelekwa katika kutekeleza miradi kwenye ngazi za chini za Serikali ionekane kupitia taarifa zitakazoandaliwa kwa kufuata sheria,kanuni,taratibu na miongozo ya fedha za Serikali iliyopo.
Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 12/6/2017 na kumalizika tarehe 13/6/2016 yalikuwa yakiendeshwa na wakufunzi ndugu Robert Mhongera( Mtaalam wa mifumo ya Kompyuta toka PS3),ndugu Audax Barongo,na ndugu Neema Beebwa(Wote ni wahasibu toka Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa) yalihudhuliwa na maafisa elimu kata ,wataalam wa afya toka hospitali ya Wilaya,na vituo vya afya kutoka kila kata.
Lengo la mafunzo hayo ilikuwa ni kuwaimarisha kiujuzi wataalam hao kuelewa mzunguko wa jumla wa udhibiti wa fedha za umma na mahusiano yanayohusu upelekaji wa fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma kama shule ,zahanati ,na vituo vya Afya.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved