Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Rubilizi, Kikukuru, Omukitembe, Kalambi na Mukunyu katika Kata ya Kikukuru wenye thamani ya bilioni 5.066 utaanza kutekelezwa hivi karibuni na mkandarasi OTONDE CONSTRUCTION & GENERAL SUPPLIES ambapo unatarajiwa ukamilike ifikapo Decemba 30, 2024.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe akiongea na wananchi, viongozi wa kiserikali na chama waliojitokeza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo ametoa onyo kwa wale watakaohujumu miundombinu ya mradi huo kwani wakibainika sheria zitachuuliwa juu yao.
Aidha, amemtaka Mkandarasi kukamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa ili uanze kutoa huduma kwa wananchi wa Kata ya Kikukuru ambao walikuwa wanakumbana na adha ya maji safi na salama kwa muda mrefu.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi, Mhandisi Kashonele Kagodoro amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa matenki 4 yenye ujazo lita 100m3, 150m3, 200m3 na 75m3, Ujenzi wa ofisi ya CBWSOs, Ununuzi wa bomba, uchimbaji wa mtaro pamoja na ulazaji wa bomba zenye urefu wa 65.23km, Ununuzi na ufungaji wa pampu 02 pamoja na ujenzi wa nyumba 02 za mitambo (pump house), Ujenzi wa DP 20 pamoja na kuunganisha huduma kwa wateja 200 waliondani ya mita 50 ya laini kuu.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved