Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mheshimiwa Rashid Mwaimu, leo amezindua mnada wa mifugo wa Katera, uliopo Wilaya ya Kyerwa.Mnada huo ambao kwa kipindi cha miaka mingi ulikuwa umesimamisha shughuli zake kutokana na sababu kadhaa umepokelewa kwa furaha na wananchi wa wilaya hii.
Akiwahutubia wananchi walioshiriki katika uzinduzi huu, Mheshimiwa Mwaimu aliwahimiza wafugaji kuleta mifugo yao katika mnada huu, ili kuuza mifugo yao kwa bei ya soko, na hivyo kujiongezea kipato kitakachoinua ufugaji wao na kuiongezea mapato Serikali ambayo itakusanya tozo kutoka kwa wanunuzi watakaofika mnadani hapo.
“Nipende kuwafahamisha wafugaji wangu wa Wilaya hii, sitakubali na wala sita sita kumchukulia hatua mtu yoyote atayetaka kuhujumu miundombinu ya mahali hapa, wala kutorosha mifugo kwenda nchi jirani pasipo kufuata taratibu” , mheshimiwa Mwaimu alisisitiza.
Aidha, siku hiyo jumla ya ng’ombe 70 walifikishwa katika mnada huo,hali ambayo inaashiria mwanzo mzuri wa uendelevu wa mnada huo ambapo utakuwa ukifanyika kila siku ya Jumanne.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved