Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mheshimiwa Zaituni Abdalla Msofe amezindua bodi ya afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa siku ya Jumanne tarehe 18/04/2023.Uzinduzi huu ulifanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Wilaya ya Kyerwa na ulihudhuriwa na viongozi wengine wa Wilaya akiwepo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kyerwa, Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Bahati Henerico, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri SACF James John.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alishuhudia mchakato wa kuchagua Mwenyekiti wa bodi ya afya ambapo ndugu Selapion B. Kasenene alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo. Wajumbe wengine waliochaguliwa ni ndugu Wegesa M. Wambura, Selapion B. Kasenene, Renatus M.Kapira, na Raifrida Nyamwizi Albert.
Bodi ya afya inajukumu na kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato na kukusanya rasilimali za kutosha kuendesha huduma za afya, pia kujadili na kurekebisha mipango ya afya na bajeti.
Bodi ya afya itadumu kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia tarehe 18/4/2023 mpaka tarehe 17/4/2023.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved