Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe, Julai 22, 2025 amefanya ziara katika Kijiji cha Mkombozi Kata ya Rukuraijo ikiwa ni mwendelezo wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Wilaya ya Kyerwa.
Akizungumza na Wananchi waliojitokeza katika Mkutano huo Mhe. Msofe amewataka wananchi wawe wanatoa taarifa mapema za changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ili zitatuliwa kabla ya kuleta madhara makubwa kwa jamii.
Amesema hayo baada ya wananchi kutoa changamoto ya uwepo wa mamba na viboko wanaotishia usalama wa Wanakijiji cha Mkombozi bila kutoa taarifa sehemu husika ili hatua za kukabliana na wanyama hao zichukuliwe pamoja na kero zingine zinazowakabili kwa kipindi kirefu.
Aidha amewataka wananchi kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na kwenda kuchagua viongozi ambao wanawataka wawaongoze katika awamu ijayo kwani ni haki yao ya kikatiba, huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi pamoja na kutunza amani ya nchi.
Aidha wananchi walihoji juu ya changamoto ya barabara zilizoharibika, ukosefu wa vitambulisho vya nida, ukosefu wa huduma ya maji na umeme, uhalifu na ukiukwaji wa sheria, mambo ambayo yalipatiwa majibu na wataalam walioambana na Mkuu wa Wilaya katika ziara hiyo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved