Mkutano wa Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa umefanyika leo tar. 17 Mei 2024 kwa ajili ya kujadili taarifa ya utekelezaji wa robo ya tatu ya kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2023/2024.
Akihutubia katika mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mhe. Bahati Henerico amesema makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka.
Amesema hadi kufikia mwezi machi 2023/2024 Halmashauri imekusanya 4,135,475,577 sawa na asilimia 125.12 ya makadirio ya mapato ya ndani na kuahidi kuendelea kusimamia vyanzo vyote vya mapato na kukusanya zaidi.
Akitoa maelekezo ya Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Katibu Tarafa wa Tarafa ya Mabira Ndugu Mussa Jumanne amewataka Waheshimiwa Madiwani kushirikiana katika kupambana na magendo ya kahawa kwani tayari kuna wananchi ambao wanavuna kahawa mbichi na kuenda kuuza nchi za nje.
Aidha ameitaka Halmashauri kupitia Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuongeza nguvu katika kukusanya mapato kupitia wafanyabiashara wa maduka ambao hawana leseni na hawalipi ushuru na hivyo kuacha mianya mingi inayopelekea Serikali kukosa mapato.
Akitolea ufafanuzi wa hoja zilizoibuliwa na Waheshimiwa Madiwani katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa SACF. James John pamoja na mambo mengine amesema Halmashauri imejiwekea utaratibu wa kujenga Zahanati mbili kila mwaka kwa kushirikiana na jamii.
Amesema kwa mwaka huu Halmashauri kwa kupitia mapato yake ya ndani na michango ya jamii inajenga Zahanati za Businde na Rwensheshe na mwaka jana Halmashauri ilijenga Zahanati za Kaina na Katera na kuwataka Waheshimiwa Madiwani kushirikiana na Serikali kwa kuwahimiza wananchi kuchangia miradi ya maendeleo.
MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WAFANYIKA KYERWA
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved