Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kyerwa, Ndugu Sacf James John amesikitishwa na hali ya uvamizi wa wananchi katika maeneo ya ardhi za vituo vya kutolea mafunzo kwa wakulima (Farmers'Extension Center-FEC) unaoendelea kutokea katika kituo cha Nkwenda.Hayo yamebainika wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi uliofanywa na Timu ya wataalam wa Halmashauri (CMT) walipotembelea mradi huo hivi karibuni.
Katika ziara hiyo, ilibainika kwa kipindi kirefu wananchi wamekuwa wakilivamia eneo la FEC Nkwenda kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na uzalishaji mali kutokana na eneo hilo kutokuwa na mipaka ya kisheria (hati ya ardhi).Hivyo, ili kudhibiti uvamizi huo, Mkurugenzi Mtendaji alimuagiza Afisa ardhi kuharakisha mchakato wa upimaji wa eneo hilo ili kupunguza migogoro isiyo na ulazima.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved