Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Ndg, Meshack Libent akikagua moja ya shamba darasa la mihogo katika miradi iliyofadhiliwa na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani, FAO. Katika kuendelea kuinua kipato pamoja na kuimarisha hali ya afya katika Wilaya ya Kyerwa FAO imeendelea kuwezesha upatikanaji wa mbegu bora za mazao yanayohimili ukame na magonjwa. FAO imewezesha mashamba darasa ya mazao ya mohogo na migomba pamoja na yale ya mifugo ya kuku na nguruwe. Zaidi ya kaya 400 zimeweza kunufaika na miradi hiyo kupitia vikundi vya uzalishaji. Wilaya ya Kyerwa inaendelea kulishukuru shirika kwa kazi kubwa inayofanya wilayani na inaendelea kuwasihi wasisite kuongeza uwezeshaji kila fursa inapotokea.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved