“Leo nina jukumu kubwa moja la kuwakabidhi mikopo vikundi vya wanawake . Mikopo hii ni katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 ya Chama cha Mapinduzi ibara ya 230 (“a” hadi “d” )” –ni kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa alipokuwa katika sherehe ya kugawa mikopo kwa vikundi 26 vya Wanawake na Vijana inayotolewa na Halmashauri.
Katika halfa hiyo, iliyohudhuliwa pia na Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Rwabwere, Mheshimiwa Bahati Henerico, jumla ya vikundi 17 vya Wanawake vilipatiwa mkopo wa shilingi 92,640,000/=,na shilingi 87,000,000/= zilikabidhiwa kwa vikundi 9 vya Vijana.
Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa imekuwa ikitenga kiasi cha 10% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kukopesha vikundi vya Wanawake, Vijana na Walemavu.Halmashauri ina jumla ya vikundi 320 vilivyosajiliwa.Kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Wilaya imetenga kiasi cha Tsh: 199,853,360.
Mheshimiwa Rashid Mwaimu( Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa) ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, aliupongeza uongozi wa Halmashauri kwa kutenga fedha kwa ajili ya Wanawake,Vijana , na Walemavu na kusisitiza kuwa uchambuzi wa Vikundi vyenye sifa ufuate miongozo iliyowekwa na Serikali ili ilete matokeo chanya kwa watakaokopeshwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved