Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa SACF. James John amewapongeza wanakijiji cha Rwakabunda kata ya Bugara kwa kutoa eneo la ekari nane kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari katika maeneo yao.
Shule hiyo itakayogharimu kiasi Tsh 584,280,028 kutoka serikalini kuu kwa ushirikiano wa Benki ya Dunia kupitia mradi wa uboreshaji wa elimu ya sekondari nchini (SEQUIP).
SACF. James amewaomba wanakijiji kushirikiana na serikali katika kutekeleza mradi huo kwani utakuwa na faida nyingi kwao kwa watoto wao kupata elimu, kupunguza umbali wanaotembea kufuata shule zingine na utafungua fursa nyingi na kupelekea maendeleo ya haraka katika kijiji hicho.
“Mkipambana tutapambana pamoja, hii ni fursa ya kuja kwa wageni kama mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, mawaziri, na wageni wengine wa kiserikali na kisiasa ambao watakuja kutatua changamoto zingine.” alisema SACF. John.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bugara Mhe. Bishanga Fredrick ameishukuru serikali na kuahidi ushirikiano wake katika kutekeleza mradi huo na kuipongeza serikali ya kijiji na wananchi kwa kushirikiana naye na kuomba ushirikiano huo uendelee ili kutekeleza mradi huo kwa wakati.
Akitoa maelezo ya awali Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kyerwa Bw. Stephano Ndabazi amesema mradi huu utajengwa kwa miezi mitatu ambapo utaanza kwa vyumba nane vya madarasa, ofisi mbili, jengo la utawala, majengo ya maabara ya kemia na fizikia, pamoja matundu nane ya vyoo. Na awamu ya pili ya zitajengwa nyumba za waalimu na ununuzi wa vifaa vya tehama.
Pia Wanakijiji cha Rwakabunda wamefurahishwa na ujio mradi huo na kuahidi wataendelea kutoa ushirikiano na kuchangia nguvu zao katika swala zima la kukamisha mradi huo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved