Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amewahamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Ametoa hamasa hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Umoja Kata ya Rwabwere ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya amesema ifikapo tarehe 29 Oktoba wananchi wote wenye sifa wanatakiwa kwenda kupiga kura ili kuchagua viongozi wanaowata wao.
"...tusifanye kosa la kusikiliza propaganda zinazoendelea tukashindwa kwenda kutekeleza haki yetu ya msingi, haki ya kikatiba ya kwenda kuchagua viongozi tunaoona watatuletea maendeleo, wewe usipoenda kuchagua utaletewa kiongozi halafu baadae utalalamika," ameeleza Mhe. Msofe.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved