Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amewataka wananchi na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Nyakakoni Kata ya Rutunguru kuachana na biashara ya magendo ya kahawa na kutorosha madini ya tini kupelekwa nchi jirani.
Amesema hayo katika ziara yake leo Tarehe 30 Mei 2024 ikiwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi katika maisha yao na kuhitaji ufumbuzi kutoka serikalini.
Mhe. Msofe amesema anasikitishwa na kitendo cha watu ambao wanaaminiwa na serikali kuhusishwa na tuhuma za kutorosha madini ya tini na kahawa na kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na kutoa taarifa za watu wanaofanya shughuli hizo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Niwaombe sana tuendelee kushirikiana tupeane taarifa, kwa maana ulinzi ni wa kwetu sote, mimi siwezi kukaa kila Kijiji au Kitongoji lakini kwa ushirikiano wenu nyinyi tunaweza kuilinda Kyerwa, tunaweza tukalinda mali zetu.
“Wapo watu wanaoendelea kuiba kahawa kwenye mashamba ya watu tena wanaiba kahawa zikiwa mbichi na kukata kabisa ile miche ya kahawa, iwapo tukimkamata mtu atakuwa mfano kwa Wilaya nzima.” Ameeleza Mhe. Msofe.
Aidha kero ya maji, barabara, umeme, upungufu wa walimu, malezi na kujichukulia sharia mkononi, uvamizi wa maeneo ya serikali ya kijiji na hifadhi ni miongoni mwa kero zilizoibuliwa na wananchi na kutolewa ufafanuzi na wataalamu kutoka Halmashauri na Taasisi za Umma katika Wilaya ya Kerwa ambao waliambatana na Mkuu wa Wilaya katika ziara hiyo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved