Mkuu wa mkoa wa Kagera,mheshimiwa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu amefanya ziara ya kawaida ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Kyerwa.Katika ziara hiyo iliyofanyika tarehe 02 februari,2018 ilikuwa mahsusi kwa ajili ya kutembelea miradi inayotekelewa kupitia sekta ya afya.Aidha akiwa na mwenyeji wake mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mheshimiwa Kanali Mstaafu Shaban I.Lisu, na viongozi wengine amekagua ujenzi wa Zahanati za Nyakashenyi,Chanya, na ukarabati wa kituo cha afya Murongo baada ya kupata shilingi milioni 400 kutoka Serikalini.
Pamoja na mambo mengine,mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliwahimiza wananchi kuhusu umuhimu wa kuanzisha ujenzi wa Zahanati kwa kila kijiji lakini pia kuhamasisha wananchi kupanda miti ya matunda kwa ajili ya kupambana na utapia mlo.Katika kusisitiza jambo hilo,mheshimiwa mkuu wa mkoa ameshiriki katika zoezi la upandaji miti katika vituo vyote vitatu (3) vya tiba alivyovitembelea.
Aidha,mkuu wa mkoa aliwahimia wananchi kujikita katika shughuli za kilimo kwani asilimia 85 ya Watanzania wanategemea kilimo kwa ajili ya kuinua kipato chao.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved