Katika mwendelezo wa mafunzo ya Watumishi wa afya ya kupambana na utapiamlo katika Wilaya ya Kyerwa, leo tarehe 16 Oktoba 2025, washiriki hao wamepatiwa mafunzo kwa vitendo katika Hospitali ya Wilaya juu ya kupambana na ugonjwa huo.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo juu ya namna bora ya kuwahudumia na kuwatibu watoto wanaokabiliwa na changamoto ya ugonjwa wa utapiamlo ikiwa ni pamoja na kuwashauri wazazi juu ya lishe bora kwa watoto.
Mafunzo hayo ya siku tano yakihusisha watumishi wa kada ya afya kutoka katika Vituo vya Afya na Hospitali ya Wilaya ya Kyerwa yameanza tarehe 13 Oktoba na yanatarajiwa kukamika tarehe 17 Oktoba 2025 yakiwa yamelenga kuwaongezea ujuzi na ufanisi wa watumishi hao katika utoaji wa huduma bora za afya kwa watoto wenye utapiamlo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved