Mafunzo hayo yametolewa kwa waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya kibayometriki (BVR) katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa leo tarehe 29 Aprili 2025.
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Kyerwa, SACF. James John amewataka wanasemina hao kuzingatia mafunzo hayo na kwenda kufanya kazi kwa ujuzi, uwezo na weledi walionao ili kutekeleza zoezi la Kitaifa la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili.
Aidha amewataka Waandikishaji hao wasihodhi zoezi hilo, kwani kama watakutana na changomoto yoyote wafanye mawasiliano na wataalam wa kutoka Kata, Jimbo au Taifa ili kuhakikisha zoezi hilo linatekelezwa kwa ufasaha katika Wilaya ya Kyerwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved