Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa imeendesha mafunzo ya mikopo ya asilimia 10% inayotolewa na serikali kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu walemavu.
Mafunzo haya yamefanyika Novemba 12, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, ambayo yaliyowajumuisha Maafisa Watendaji wa Kata, Maafisa elimu Kata, Maafisa kilimo, Polisi Kata, Maafisa Maendeleo ya Jamii, na Maafisa Afya kutoka katika kata zote 24 za Kyerwa.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kuunda vikundi vyenye sifa ya kupata mikopo, kuvifanyia tathimini, kuvisajili, na namna ya ufuatiliaji wa mikopo ya 10%.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved