Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa leo tar. 6 Desemba 2023 wameanza kupatiwa mafunzo ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa Upimaji Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (PERMIS & PIPMIS) na tathmini ya mahitaji ya Rasilimali Watu (Human Resources Assessment System).
Mkurugenzi Msaidizi-Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Jeanfrida Mushumbuzi akiongoza mafunzo hayo, amesema kuwa mfumo utatumika kupima utendaji kazi wa watumishi wa umma na baada ya mafunzo hayo kila mtumishi atatakiwa kutumia mfumo huo kutokana na kazi ambazo ameziweka kutokana na kalenda ya mwaka mzima.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Mkuu wa Idara ya Utumishi na Rasilimali Watu Bw. Henerica Rushala amewataka washiriki wote kizingatia mafunzo hayo kwani ni muhimu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved