Wilaya ya Kyerwa inatarajia kushiriki zoezi la kampeni ya utoaji chanjo dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kwa watoto wa kike kuanzia miaka Tisa hadi kumi na nne wapatao 38,009 kwa lengo la kuwakinga na ugonjwa huo hatarishi kwenye jamii.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha kamati ya afya ya msingi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa kwa kujumuisha Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wataalamu wa Idara ya afya na Halmashauri, Viongozi wa Dini na baadhi ya wadau wa maendeleo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe baada ya kupokea taarifa ya kampeini ya utoaji chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi amewataka wajumbe wa kamati hiyo kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri katika jamii na kuwataka Viongozi wa Dini kutumia miskiti na makanisa kueleza umuhimu wa chanjo hiyo ambayo Haina madhara yoyote bali inaokoa nguvu kazi ya taifa.
Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa afya ni muhimu kuliko vitu vingine hivyo wazazi, na jamii nzima inapatiwa elimu naihakikishe mabinti zao wanapatiwa chanjo ili waelewe lengo la serikali kuwa ni zuri kwa jamii.
Awali akielezea mpango wa Kampeni hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Lewanga Msafiri amesema chanjo hiyo kupitia maalumu itaanza kufanyika Tar. 22-26 Aprili 2024 na itakuwa endelevu Huku akibainisha madhara ya ugonjwa huo ambao unaathiri watu wa rika zote licha ya kuwashambulia zaidi wanawake wa kuanzia umri wa miaka 34 adi 45 ambapo dalili kubwa ni kutoka uchafu ukeni na wenye harufu.
Sambamba na hayo amesema zipo timu za wataalamu zitakazopita maeneo ya jamii zikiwemo shule na kwenye vituo vya afya ambapo chanjo itatolewa kwa mabinti hao na baada ya tr 26 zoezi litakuwa endelevu na litakuwa linatolewa katika Vituo vya Afya mpaka mwishoni mwa mwaka huu na ifikapo Januari 2025 itaanza kutolewa kwa mabinti wa miaka tisa tu.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved