Katika kuelekea uzinduzi wa daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza tarehe 05 hadi 11 Agosti 2024 katika Mkoa wa Kagera, Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kyerwa SACF. James John amefunga mafunzo ya Uandikishaji kwa maafisa waandikishaji ngazi ya Kata.
Amewaasa kuzingatia mafunzo waliyoyapata ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na kushirikiana katika kazi zao ili kufanikisha zoezi hili.
Amewasisitiza maafisa hao kuzingatia maadili ya kazi, kufanya kazi kwa weledi na wakikutana na changamoto yoyote wawasiliane na wasimamizi wa kata au jimbo ili kuweza kutatua changamoto hizo.
Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika kitarafa katika Wilaya ya Kyerwa ambazo ni Tarafa ya Kaisho, Nkwenda, Murongo na Mabira ambayo yamehusisha ujazaji wa fomu, kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura pamoja na matumizi sahihi ya vifaa vitakavyotumika katika zoezi hilo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved