Kamati ya Maafa Wilaya ya Kyerwa yajengewa uwezo. Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Kyerwa imeshiriki mafunzo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na Maafa mbalimbali yanayoweza kujitokeza leo tarehe 17.8/2018. Mafunzo hayo yametolewa na wataalamu kutoka ofisi ya Katibu Tawala Mkoa Kagera kwa kushirikiana na wataalamu wa Shirika la Kilimo na Chakula Duniani, FAO. Aidha katika mafunzo hayo Wanakamti wameweza kufahamu dhana ya Maafa kwa ujumla, Sheria ya Maafa Na. 7 ya mwaka 2015, Muundo wa Kamati za Maafa kuanzia ngazi ya Taifa mpaka kijiji na majukumu ya Kamati hizo kwa Upana wake. Mafunzo haya yanalenga kuwaweka tayari wananchi kupitia Kamati hizo kukabiliana na maafa mbalimbali ikiwemo Mafuriko, vimbunga, moto, Tetemeko nk. Aidha Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Ndg. Thomas Mahenge aliwashukuru wawezeshaji kwa kuijengea uwezo Kamati hiyo na kuahidi kuyasimamia vizuri na kutumia elimu hiyo kama inavyotarajiwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved