Wilaya ya Kyerwa imefanikiwa kushika nafasi ya tatu (3) kimkoa katika michezo ya wanafunzi kwa shule za sekondari (UMISSETA) mkoani Kagera.Mashindano haya yaliyofanyika katika chuo cha ualimu Katoka katika Wilaya ya Muleba yalishirikisha Wilaya za Muleba,Ngara,Bukoba,Kyerwa,Biharamulo,Karangwe,na Missenyi.Michezo hii ambayo ilianza tarehe 25-29/05/2017 ilihusisha michezo ya mpira wa kikapu,mpira wa wavu,riadha(mbio za mita 100-3000) na mchezo wa mitupo.
Wilaya ya Kyerwa katika mashindano haya ilipeleka jumla ya wanafunzi 35,kati yao wanafunzi 13 wamefanikiwa kushinda katika nafasi kati ya namba moja hadi mshindi namba tatu,ambapo wanafunzi hawa wamefanikiwa kuendelea kwa hatua ya UMISSETA ngazi ya Taifa itakayofanyika tarehe 5-17/06/2017 katika chuo cha ualimu Butimba mkoani Mwanza.
Majina ya wanafunzi hao walioiwakilisha vyema na kupata fursa ya kusonga mbele ni pamoja na Eliud Ndamukaka(Kaisho sekondari),Sadot Anatory(Kaisho Sekondari),Horance Thomas (Kaisho Sekondari),Aaron Gaspar(Kaisho Sekondari),Darius William(Kaisho Sekondari),Princel Julius (Isingiro Sekondari),Happiness Deusdedit(Mabira Sekondari),Anitha Dagobert(Nyamilima Sekondari),Martina Mathayo(Isingiro Sekondari),Renis Gerard(Chitwe Sekondari),Tumain Tomuson(Kaisho Sekondari) na Leah Anselimu(Nakake Sekondari).
Washindi wa jumla kiwilaya ni Muleba (nafasi ya kwanza), Missenyi (nafasi ya pili), na Kyerwa (nafasi ya tatu)
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved