Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Amesema hayo katika mkutano maalumu wa baraza la madiwani la kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa leo Juni 17, 2025.
"Nichukue nafasi hii kuwapongeza sana kwa kupata hati safi katika ukaguzi wa hesabu za serikali katika mwaka wa fefha 2023/24, hongereni sana."amesema Mhe. Hajjat Mwassa.
Vile vile Mkuu wa Mkoa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato katika mwaka wa fedha wa 2024/2025 ambapo Halmashauri imekusanya bilioni 6.9 sawa na 112% ya lengo la Mwaka ambalo ni lilikiwa bilioni 6.1.
"Natambua kwamba mapato haya kwa kiasi kikubwa yameongezeka kutokana na ongezeko la bei ya kahawa, sasa basi kama ndivyo ilivyo nasi tuongeze uzalishaji wa kahawa ili tuendelee kufanya vizuri.
"Lakini pia tuongeze udhibiti wa utoroshaji wa kahawa, mwaka jana kulikuwa na kelele nyingi sana na sisi tukaziba masikio ... lakini matokeo yake ndio haya mmeyaona wenyewe. Tunapodhibiti mapato haya, kodi inabaki kwetu na ndio zinazorudi katika miradi ya maendeleo." Ameeleza Mhe. Mwassa.
Aidha Mhe. Hajjat Mwassa amewataka Wataalamu wa Halmashauri kuzingatia matumizi ya mfumo wa ukusanyaji mapato, TAUSI, mfumo wa udhibiti wa manunuzi NeST na kuhakikisha hoja zote zinazotokana na mifumo hiyo pamoja na hoja zote zinashughulikiwa na kufungwa kwani ndoto yake ni kuongoza mkoa usio na hoja.
Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ilikuwa na hoja 28 ambapo 12 za mwaka 2023/2024, sita zimetekelezwa na kufungwa huku zingine zikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji na hoja za nyuma zilikuwa 16 ambapo nne zimetekelezwa na kufungwa na 12 ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved