“Najiuliza kwa miezi sita kama tumevuka lengo inamaana tunaweza kukusanya mara mbili na zaidi ya tulichokuwa tumejipangia, kama miezi sita tumeweza kufikia asilimia 104 imaana tumejipangia kiwango cha chini, hilo likaangaliwe, hichi kiwango tunachojipangia sio stahili yetu, sisi tunauwezo zaidi ya hapo.”
Ni kauli iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe wakati akitoa maelekezo ya serikali katika baraza la Madiwani lililofanyika leo Februari 01, 2024 katika ukumbi wa Rweru Plaza Wilaya ya Kyerwa.
Mhe. Msofe amesema kunavyanzo vingi vya mapato ambavyo havijasimamiwa vizuri na endapo vitasimamiwa kikamilifu Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa inaweza kukusanya mapato mengi zaidi na hivyo kuwataka wahusika kuongeza juhudi katika usimamizi na ukusanyaji katika vyanzo hivyo na kuibua vyanzo vingine vya mapato.
Aidha amewatahadharisha wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani kuna vyombo vinavyohusika kutoa haki na kuwataka wananchi kuenda katika vyombo hivyo ili wakapatiwe haki zao
Kwa upande mwingine amewataka Waheshimiwa Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji ambao wanashindwa kufanyakazi na Watendaji wa Kata na Vijiji na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji kuwahamisha vituo vya kazi kwa kushindwa kuelewana nao wajitathmini na waache tabia hiyo mara moja kwani imekuwa ikifanyika kwa maslahi ya watu binafsi na sio kwa maslahi ya umma.
Akipokea maelekezo ya Serikali, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mhe. Bahati Henerico amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Halmashauri na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji kuchukua hatua kwa baadhi ya Watendaji ambao sio waadilifu.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved