Wilaya ya Kyerwa imeadhimisha siku ya Malaria Duniani kwa kutoa elimu kupitia matamasha na mikutano kwenye Kata za Nkwenda,Rwabwere na Iteera.
Akizungumza na Afisa Habari wa Halmashauri, mratibu wa Malaria Wilayani, ndugu Goreth Zilyahuramu amesema kuwa kwa kushirikiana na programu ya Shinda Malaria , wameweza kuwafikia wanajamii wa kata 3 za NKwenda,Rwabwere,na Iteera ambapo wametoa elimu juu ya masuala ya kujikinga na ugonjwa wa Malaria. "Tunawashukuru wadau hawa ambao wamejumuika nasi katika kuadhimisha siku hii kwa kutoa elimu kwa awananchi wa Kyerwa" alisisitiza Ndugu Goreth.
Siku ya Malaria Duniani huadhimishwa kila tarehe 25 , na kauli mbiu ya mwaka huu ni wakati wa kutokomeza malaria ni sasa:badilika, wekeza, tekeleza. Ziro malaria inaanza na mimi.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved