Maadhimisho ya siku ya mashujaa Wilaya ya Kyewa yamefanyika kwa watumishi wa taasisi za Umma kufanya shughuli za usafi wa mazingira na kupanda miti katika maeneo ya Shule ya Sekonari Kyerwa Modern na Hospitali ya Wilaya.
Katibu Tawala wa Wilaya Bw. Mussa Gumbo akiongoza shughuli hiyo, akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri SACF. James John pamoja na watumishi Halmashauri ya Wilaya, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya RUWASA, Ofisi ya TARURA, na Ofisi ya TFS ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya siku muhumu ya kuwaenzi mashujaa wa Taifa la Tanzania.
Katika hotuba yake Bw. Gumbo amewataka watumishi wa Wilaya ya Kyerwa kuendelea kushirikiana, kudumisha uzalendo, amani, upendo na kuendelea kuwaenzi mashujaa wetu waliopoteza uhai wao katika kupigania Taifa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved