Novemba 7, 2025 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Dkt. Lewanga Msafiri amefungua mafunzo maalum ya kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa chini ya umri wa miaka mitano.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa yakiwahusisha Maafisa Ustawi wa Jamii na watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuwajengea uwezo wa kwenda kuhakikisha watoto wote wanaozaliwa katika vituo vyao wanapatiwa vyeti vyao.
"Moja wapo ya haki ya msingi ya mtoto ni kuishi pamoja na kutambuliwa kuwa yeye ni raia wa nchi gani, amezaliwa tarehe ngapi, pamoja na haki zake zote za msingi kama binadamu.
"Unapo mhudumia mama aliyejifungua na ukaacha kumsajili mtoto na kumpatia cheti cha kuzaliwa, unakuwa unamnyima mtoto huyo haki yake ya msingi." ameeleza Dkt. Lewanga.
Naye Ndg. Albert Sitini, Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa amesema kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watoa huduma juu ya kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa kila watoto wanayezaliwa kwenye vituo vyao.
"Hapo awali kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa hivyo Serikali imeweza kurahisisha zoezi hili kwa kuwapa jukumu hili Maafisa Ustawi wa Jamii ili waweze kusajili vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa chini ya miaka mitano." ameeleza Ndg. Sitini.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved