Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mh. Rashid Mwahimu akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wataalam wa Idara ya Afya wakiongozwa na Mganga Mkuu wa Wilaya Dr Diocles Ngaiza wakikabidhiwa vifaa Tiba kwa ajili ya Kituo cha Afya Murongo.
Vifaa hivi ni msaada kutoka katika Kampuni ya mradi wa ujenzi wa Bwawa la kufua Umeme Kyerwa kutoka Mto Kagera ya "KIKAGATE POWER PROJECT". Hii ni sehemu ya "Social Responsibility" ya Mradi huu.
Vifaa vilivyopokelewa ni pamoja na:
1. Vitanda vya wagonjwa 49
2. Magodoro 49
3. Mashuka 98
4. Blanket 49
5. B.p Mashine 5
6. Pulse Oxymetry 5
Pamoja na vifaa hivi, wadau hawa wametoa pia Msaada wa Matenki 2 ya kuvuna maji ya mvua yenye ujazo wa Lita 10,000 kwa ajili ya kituo cha Afya Murongo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved