Kikao Cha kisheria Cha Kamati ya ushauri ya Wilaya ya Kyerwa kimefanyika Leo Desemba 02, 2024 na kukutanisha Viongozi wa Serikali, Taasisi, Wataalamu, Viongozi wa dini pamoja na Viongozi wa Vyama vya siasa
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe ameongoza kikao hicho kilichojadili taarifa mbalimbali zilizotekelezwa na taasisi za Serikali katika Wilaya ya Kyerwa.
Katika Kikao hiki, tasisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, TARURA, TANESCO na RUWASA zimewasilisha taarifa za utekelezaji zinazoonesha malengo, mafanikio pamoja na changamoto zinazowakabili Wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Baada ya mawasilisho hayo, wajumbe walichangia mada kwa kutoa maoni yao ambapo Idara husika ziliyapokea na kuahidi kuyafanyia kazi.
Mwenyekiti alisema kuwa milango ya Ofisi yake ipo wazi na muda wote, mwananchi au Kiongozi anakaribishwa kwa majadiliano zaidi kwa manufaa ya Maendeleo ya Wilaya ya Kyerwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved