MKUU wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amefungua mafunzo ya siku tatu ya usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa wasajili wasaidizi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa CCM wilayani hapo yakitolewa na wataalamu kutoka RITA makao makuu ya Taifa Tanzania Bara, RITA Mkoa wa Kagera na wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Kyerwa yenye lengo la kuwajengea uwezo wasajili wasaidizi ambao ni watendaji wa kata, waganga wafawidhi na watoa huduma za afya kutoka katika zahanati, vituo vya afya na hospitali katika wilaya ya Kyerwa.
Mhe. Msofe amewataka wale wote ambao wataenda kushiriki katika zoezi hili wakafanyekazi kizalendo na kwa bidii ili wasiache mtoto yeyote aliyechini ya umri wa miaka mitano katika wilaa hii.
“Tujitahidi tusiache mtu nyuma, tuhakikishe tunawasajili watoto wote na kazi hii ifanyika kwa uadilifu mkubwa ukizingatia sisi tuko mipakani.” Alisema Mhe. Msofe.
Aidha amesisitiza na kuwataka wasajili wasaidizi wakawe makini na kuepuka kukosea majina na taarifa za watoto watakao wasajili ili kuepusha usumbufu hapo baadaye.
Baada ya kufunguliwa kwa mafunzo hayo, wawezeshaji kutoka RITA na Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa wameanza rasmi zoezi la kuwafundisha wasajili wasaidizi namna ya kujaza faarifa za watoto katika makabrasha na kuelezwa vitu vya muhimu ambavyo vinahitajika ili kuweza kumsajili mtoto na kumpatia cheti cha kuzaliwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved