Watumishi wa taasisi za umma zilizopo Wilayani Kyerwa,leo hii wamepatiwa mafunzo juu ya sheria,kanuni na taratibu za utumishi wa umma kutoka ofisi ya Rais Ikulu katibu Mkuu Kiongozi.
Mafunzo haya yaliyoendeshwa na wataalam wa Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi,ndugu Fransis Mangira ambaye ni mratibu wa utawala ,na ndugu Abdalah Said Mangare ambaye ni mratibu msaidizi utawala yalijikita katika kuwajengea uwezo watumishi wa umma kutambua sheria,kanuni,taratibu,na miongozo mbali mbali katika kuhudumia wananchi.
Aidha,katika kusisitiza ndugu Fransis Mangira,aliwasilisha maagizo matano mahsusi toka kwa ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi kwa watumishi wote kama ifuatavyo:-
Pia ndugu Mangira aliwasisitiza watumishi kujitambua kwamba wao ni kundi dogo la wananchi wenye taaluma ,uzoefu,na weledi waliobatika kupata nafasi ya kuwahudumia wananchi walio wengi kwa niaba yao.Naye ndugu Abdalah Mangira,akiwasilisha maada aliwata watumishi kufanya vikao vya watumishi ili kuondoa changamoto mbalimbali za kiutumishi,kufuatilia utendaji wa watumishi waliopo ngazi za chini,kuheshimu mamlaka,madaraka na mipaka ya majukumu,kuzigatia maadili ya utendaji wa kazi, na kufuata namna bora ya mawasiliano serikalini.Katika kuahirisha kikao kazi hicho, katibu tawala Wilaya,mheshimiwa Gyeson Mwengu aliwasisitiza watumishi kuvisaidia vyombo vya ulinzi na usalama kutoa taarifa juu ya wahamiaji haramu wanaoingia nchini katika vyombo vya dola.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved