KAMATI ya Siasa ya Wilaya ya Kyerwa imefanya ziara leo, Februari 14, 2025 kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya na kuridhishwa na usimamizi wa miradi hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kyerwa, Ndugu Daniel Damian, amempongeza Mkuu wa Wilaya Mhe. Zaituni Msofe, Mwenyekiti wa Halmashuari Mhe. Bahati Henerico, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri SACF. James John pamoja na Wataalam wote wanaosimamia miradi hiyo akibainisha kuwa itaongeza fursa kwa wananchi na kuchochea maendeleo kwa Wilaya ya Kyerwa.
Aidha, Ndugu Daniel amehimiza suala la upandaji miti pamoja na kutengeneza bustani katika maeneo yanayozunguka miradi hiyo ili kutunza na kupendezesha mazingira katika maeneo hayo.
Miradi iliyotembelewa ni; Ujenzi wa jengo la Baba, Mama na Mtoto katika Zahanati ya Rukuraijo (80,000,000.00), Ujenzi wa Wodi ya Magonjwa Mchanganyiko Kituo cha Nkwenda (230,000,000.00), Mradi wa maji Rubilizi-Kikukuru (5,066,000,000.00), Ujenzi wa shule ya Sekondari mpya ya Ishaka-Isingiro (584,280,029.00) na Ujenzi wa shule ya Awali na Msingi mpya ya mchapuo wa kingereza-Kyerwa (300,000,000.00).
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved