Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kyerwa leo tar. 15 Februari 2024 imetembelea na kukagua miradi mitano ya maendeleo na kuridhishwa na utekelezaji wa ilani ya chama kwa mwaka 2020 hadi 2025.
Akiongoza ziara hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kyerwa Ndg. Daniel Damiani amesema ameridhishwa na usimamizi wa miradi ambayo inatekelezwa na Serikali katika Wilaya ya Kyerwa huku akitoa maelekezo kwa kila mradi uliotembelewa na kukaguliwa.
Katika mradi wa Mwalo wa Samaki wa Katwe uliopo katika Kata ya Isingiro, kamati imeridhwa na usimamizi wa mwalo huo unaofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa na Serikali ya Kijiji huku ikitoa maelekezo kwa serikali kuhakikisha wavuvi wanawekewa mazingira mazuri ya barabara na kuboreshewa huduma za kijamii.
Vile vile Kamati imeipongeza Serikali kwa hali ya kuripoti wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari ya Isingiro ambapo mpaka sasa wameripoti wanafunzi 283 ambayo sawa na asilimia 94 na kutoa rai kwa Serikali kufuatilia na kuhakikisha waliobaki wanaripoti shuleni.
Katika ukaguzi wa Barabara ya Anza Kuelimisha (KM 2.1) iliyoko Kata ya Kaisho inayogharimu kiasi Tsh. 32,990,880 inayojengwa kwa kiwango cha changarawe. Kamati imeipongeza Serikali na mkandarasi wa mradi huo DRK Merchants kwa kusimamia mradi huo kwa gharama nafuu.
Aidha katika mradi wa shule ya Msingi Rwesinga kata ya Rutunguru kamati imetembelea ujenzi wa vyoo matundu 27 ambayo yako katika hatua mbalimbali za umaliziaji na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.
Pia Kamati ilitembelea mradi wa Kituo cha Afya Rutunguru na kuridhishwa na huduma zinazotolewa kituoni hapo na kutoa maelekezo kwa Serikali kuhakikisha umeme unaunganishwa katika kituo hicho ili kuboresha huduma.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved