Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi yatembelea na kukagua miradi ya Maendeleo. Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi wilayani Kyerwa kikiongozwa na Katibu wake Wilaya ya Kyerwa imetembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha Januari- Desemba, 2018. Hii ni kwa ajili ya kukagua na kujionea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Chama Tawala. Katika kukagua miradi hiyo kamati imetembelea miradi ya Ujenzi wa Zahanati, madarasa na miradi ya maji. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Chanya, Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kamuli, Ujenzi wa madarasa Shule ya Msingi Omukachili, Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Murongo na mradi wa maji Kaisho-Isingiro. Miradi yote iliyotembelewa ilikuwa katika hatua nzuri na viongozi wa Chama wameipongeza Serikali kwa utekelezaji wa Ilani ya Chama pamoja na changamoto ndogo zilizojitokeza.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved