Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Kyerwa imekutana tarehe 3/7/2018 kujadili utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe zilizopangwa kutekelezwa katika kipindi cha robo ya pili (Sept-Dis). Akiongea katika kikao hicho, Mratibu wa Shirika la IMA Mkoa (Linalofadhili shughuli za lishe Mkoani Kagera) aliwaomba wajumbe kuendelea kusambaza elimu ya Lishe kwa Jamii. Hii itapelekea kupungua kwa tatizo la utapiamlo na udumavu hasa kwa watoto wa chini ya umri wa miaka miwili. Aidha Mkurugenzi Mtendaji alitumia fursa hii pia kumsisitiza Afisa Mipango kuendelea kutenga bajeti kwa ajili ya shughuliza lishe Wilayani. "Utapiamlo limekuwa tatizo kubwa ndani ya Halmashauri yetu kama takwimu zinavyoonesha, hii inapelekea ugumu hata wakati wa kuwafundisha wanafunzi darasani. Siyo wanafunzi tu bali hata watu wazima katika ofisi zetu wamekuwa wagumu katika utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya serikali, wengine ni kwa kuwa hawakupata lishe bora hivyo kupata udumavu wa akili" alisisitiza Mkurugenzi. Kikao hicho kilimalizika kwa wajumbe kukubaliana juu ya utekelezaji wa shughuli za lishe.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved