Kamati ya Fedha,Uongozi,na Mipango (FUM) ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa haijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo la ofisi za Halmashauri.Hayo yalibainika wakati kamati hii ilipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri mnamo tarehe 26 Oktoba,2017.Baadhi ya mapungufu yaliyobainika ni kuwa mkandarasi amechelewa sana kuanza ujenzi,pia kasi ya ujenzi inaonekana kuwa ndogo kwa ni vitendea kazi vilivyopo eneo la mradi haviendani na ukubwa wa mradi.
Mradi huu ambao unagharimu kiasi cha shilingi 750,000,000 kwa awamu ya kwanza ikiwa ni kujenga msingi,na ghorofa ya chini(Ground floor).Mpaka kukamilika mradi huu unatarajiwa kutumia kiasi cha takribani shilingi bilioni tatu na ushee,ikiwa na ghorofa tatu za jengo la utawala na ukumbi wa mikutano.
Aidha,katika ziara hiyo kamati pia ilitembelea ukarabati na upanuzi wa mradi wa maji Kagenyi na Rukulaijo wenye gharama ya Tsh.127,008,081 unaofadhiliwa na WSDP,mradi wa maji Iteera wenye gharama ya Tsh.837,538,000 unaofadhiliwa na WSDP,mradi wa kuezeka vyumba 2 vya madarasa na ofisi ya walimu shule ya msingi Rwanyango wenye gharama ya Tsh. 23,700,000 unaofadhiliwa na CDCF na CDG,ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa shule ya sekondari Mabira wenye thamani ya Tsh 60,000,000 unaofadhiliwa na P4R na CDG,kurudisha na kukarabati miundombinu iliyoaribiwa na tetemeko la ardhi shule ya msingi Ileega yenye gharama ya Tsh.111,202,000 unaofadhiliwa na Mfuko wa Maafa,kurudisha na kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi shule ya msingi Nyamilima yenye gharama ya Tsh. 60,000,000 unaofadhiliwa na Mfuko wa Maafa,Ujenzi wa zahanati ya Rwele yenye gharama ya Tsh.125,345,330 unaofadhiliwa na Mfuko wa Maafa,ujenzi wa mradi wa kusambaza maji Rwenkorongo/Rubwera Tsh. 234,218,003 unaofadhiliwa na WSDP,ujenzi wa ofisi ya kata Kaisho wenye gharama ya Tsh. 18,000,000 unaofadhiliwa na CDG,mradi wa ukarabati na upanuzi wa mradi wa maji Kaisho/Isingiro/Rutunguru wenye thamani ya Tsh.649,345,866 unaofadhiliwa na WSDP,mradi wa ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa shule ya msingi Rutunguru wenye gharama ya Tsh.5,850,000 unaofadhiliwa na Mfuko wa Jimbo(CDCF),ujenzi wa ofisi ya kata Murongo Tsh.17,343,375 unaofadhiliwa na CDG,ujenzi wa ofisi ya kijiji Murongo Tsh.28,927,000 unaofadhiliwa na Fidia ya mradi wa umeme-Murongo,ujenzi wa vyumba 3 vya maabara shule ya sekondari Murongo Tsh.18,000,000 unaofadhiliwa na CDG,na ukamilishaji wa ujenzi wa mradi wa maji mtiririko unaotumia nishati ya diseli wenye thamani ya Tsh.1,226,827,965 unaofadhiliwa na WSDP.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved