Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi katika Wilaya ya Kyerwa kimefanyika leo tar. 22 Nov. 2023 katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kujadili mpango wa kampeni ya umezeshaji wa dawa za kudhibiti Kichocho na Minyoo ya Tumbo kwa watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 14.
Kampeni hii itaanza tarehe 25 hadi 27 Novemba 2023 na inategemewa kuwafikia walengwa 81,149 ambao watapewa dawa hizo katika Kata zote za Wilaya ya Kyerwa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe Zaituni Msofe amewataka waratibu kuwa mabalozi wazuri kwa kwenda kuelimisha jamii iliyopo na waweze kushiriki kikamilifu katika zoezi hili.
Aidha amesisitiza swala la usafi lichukuliwe ‘serious’ kwa kuelimisha jamii kufuata kanuni za afya ikiwa pamoja na kupambana na imani potofu kwa wazazi ambao wanawazuia watoto wao kuywa dawa hizo ili kujikwamua na maradhi ya kichocho na minyoo ya tumbo katika Wilaya ya Kyerwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved