Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa imefanikiwa kuanzisha huduma za upasuaji wa dharula kwa Wajawazito katika kituo cha Afya Murongo mnamo tarehe 04.02.2020. Hadi kufikia tarehe 12.02.2020 jumla ya Wajawazito 9 wamekwishafanyiwa upasuaji na wote wametoka salama pamoja na watoto wao.
Kabla ya kuanzisha huduma hizi, Halmashauri ilifanya yafuatayo; Kuwasomesha watumishi 2 kozi ya kutoa Dawa za usingizi,Kufunga umeme wa Three phase katika kituo cha Afya Murongo, kufunga Tanks kubwa 3 zenye ujazo wa lita 25,000 za kuvuna maji ya mvua, na Kununua vifaa tiba pamoja na dawa kutoka MSD lakini kupokea vifaa tiba na dawa moja kwa moja toka MSD kwa fedha zilizowekwa na Serikali. Vifaa hivi ni pamoja na Generator kubwa yenye uwezo wa kuwasha umeme kituo kizima.
Aidha,katika Halmashauri kituo hiki ni cha pili baada ya kuanzisha huduma kama hizi katika kituo cha Afya Nkwenda mnamo tarehe 27.07.2016. Baada ya kuanzisha huduma hizi katika Kituo cha Nkwenda, kwa sasa jumla ya Wajawazito 350 hadi 400 wanajifungua kwa mwezi huku 60 - 70 wakifanyiwa huduma za upasuaji.
Hata hivyo, pamoja na mafanikio haya, halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi hasa Madaktari na Manesi. Kwa sasa kuna upungufu wa watumishi kwa takribani asilimia 70%.
.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved