Waziri wa Afya nchini, Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu amefanya ziara ya kikaguzi katika Wilaya ya Kyerwa,ili kujiridhisha na utayari wa serikali katika kupambana na Ugonjwa wa Ebola usiweze kuingia nchini.Akiwa katika mpaka wa Murongo unaotenganisha kati ya Nchi ya Tanzania na Uganda
alipata wasaa wa kuongea na wananchi katika soko la Ndizi la Murongo ambalo huwakutanisha wafanyabiashara wa pande mbili za nchi hizo.
Waziri Ummy alisema "Serikali ya Rais Samia itafanya juhudi zote usiku na Mchana kuhakikisha kwamba ugonjwa huu hauingii nchini, hatutalala,hatutapunzika, tutahamasishana, tutaelemishana,tutashirikishana na tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha ugonjwa huu hauingii nchini.Gharama za za Ugonjwa kuingia ni kubwa zaidi kuliko gharama za ugonjwa kutoingia nchini."
Aidha,Mheshimiwa Rashid Mwaimu alisema kuwa ameishaelekeza kuwa mgeni yoyote anayeingia nchini lazima ajiorodheshe kwenye daftari la wageni huku mpakani, ili kuhakikisha ulinzi na usalama katika mipaka yetu upo vizuri. Pia Wilaya, iliomba vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Ebola kwa watoa Huduma yaani "PPE" ambapo kupitia Bohari ya Dawa Nchi (MSD) baadhi ya vifaa vilitolewa na msaada zaidi iliahidiwa kuletwa hususani kwa Mkoa wa Kagera.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved