Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa imepokea Vitanda 100 na Mizani 10 za kupimia uzito vitakavyotumika katika Hospitali ya Wilaya ya Kyerwa vyenye thamini ya shilingi 72,800,000 kutoka serikali kuu.
Akipokea vifaa hivyo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Dkt. Lewanga Msafiri amesema vifaa hivyo vitasaidia kuondoa msongamano wa wagonjwa ambao ulikuwa unasababishwa na uhaba wa vitanda katika hospitali hiyo.
Aidha ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuwezesha huduma za afya kwani Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa imetengewa 350,000,000 kutoka serikali kuu kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya ikiwemo vifaa tiba pamoja na dawa.
“Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa ujumla inauhitaji wa Vitanda 410 na kwa hospitali ya wilaya vinahitajika vitanda 200. Kufika kwa vitanda hivi 100 maana yake bado tunauhitaji wa vitanda 310, lakini tunajua serikali yetu ni sikivu, vimekuja hivi vya awamu ya kwanza na vitafuatiwa na awami nyingine ya pili na hata ya tatu.” Alieleza Dkt. Msafiri
Kwa upande wake Afisa Huduma kwa Wateja MSD kanda ya Kagera Bi. Julieth Msele amesema wameleta vitanda hivi ikiwa ni mpango wa serikali kuu kuendelea kutoa vifaa tiba na dawa katika hospitali za kanda ya Kagera ili kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved