Katika mwendelezo wa kutembelea na kufanya mikutano ya hadhara na wananchi yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe leo Novemba 21, 2023 amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Kakanja.
Pamoja na kusikiliza kero za wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa amewaonya wazazi ambao hutorosha watoto wao pindi wanapohitimu darasa la saba na kupeleka taarifa za uongo za kupotea kwa watoto wao kituo cha polisi ili wasiende kujiunga na elimu ya sekondari.
“Mtoto wako anatakiwa kuwa shuleni wewe utuambie amepotea maana yake… OCD hizo 'loss report' za Januari za watoto wa ‘form one’ usipokee, hakuna 'loss report' itayopokelewa kwamba mtoto amepotea, hiyo hatutakubali na ni kwanini wapotee watoto wa ‘form one’ tu wengine wasipotee… mzazi utawajibika ikifika Januari tunataka watoto waliochaguliwa wawepo shuleni.” Amesema Mhe. Msofe.
Awali akisoma taarifa ya Kata, Mtendaji wa Kata ya Kakanja Bi. Maria Nyamoga amesema katika Kata ya Kakanja kuna miradi yenye thamani ya Shilingi 100,700,000/= inayotekelezwa katika mwaka huu na serikali ambayo ni pamoja na ujenzi wa miradi ya vituo vya tiba na elimu.
Katika ziara ya hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa aliambatana na Katibu Kaimu Tawala wa Wilaya, kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Viongozi wa Ulinzi na Usalama pamoja na wataalamu kutoka Halimashauri ya Wilaya ya Kyerwa, TARURA, RUWASA na TANESCO.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved