• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Kyerwa District Council
Kyerwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa

  • Mwanzo
  • kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Kata
      • Kata zetu
  • Fursa za uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda
  • huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya picha
    • Huotuba za Viongozi
    • Video

Flarence Rugimbana achaguliwa muhula wa pili kuwa Makamu Mwenyekiti baraza la Madiwani Kyerwa

Imewekwa tarehe: August 28th, 2022

Diwani wa kata ya Mabira, Mheshimiwa  Flarence Rugimbana (CCM), amechaguliwa kwa mara ya pili kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika baraza la Madiwani Halmashauri ya Kyerwa.Uchaguzi huo uliokuwa huru na wa haki umefanyika hivi  karibuni katika kikao cha Baraza la madiwani ambapo mheshimiwa Rugimbana alipata kura 25 dhidi ya kura 4 za mpinzani wake Mheshimiwa Ndibasa  (CHADEMA).

Akizungumza wakati wa kuomba kura kwa wajumbe wa Baraza, Mheshimiwa Rugimbana  kupitia chama cha Mapnduzi  (CCM) alisema “Waheshimiwa Madiwani, kazi iliyofanyika kwa kipindi cha mwaka mmoja mmeiona, na mafanikio mmeyaona, naombeni nafasi tena nimalizie kazi tuliyoianza”. Naye  Mheshimiwa Ndibasa aliyeomba kura kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alishukuru Timu ya Menejimenti kwa kuendesha uchaguzi kwa uhuru na Haki na kuwaomba wajumbe kupitia vyama vyote wampe ridhaa ya kuwa Makamu Mwenyekiti, kwani maendeleo hayana chama.

Baada ya uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti, ulifuata uchaguzi wa wajumbe wa kamati mbalimbali ambapo Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira, mheshimiwa Joel , Diwani wa Kata ya Nyaruzumbura, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati. Mheshimiwa Jonas Vedasto Diwani wa Kata ya Kamuli alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, na Mheshimiwa Beneth Byarufu, Diwani wa Kata ya Kimuli alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili.
Aidha, kwa mujibu wa Kanuni , wenyeviti wa kamati wanaingia kamati ya Fedha na Mipango moja kwa moja na pia kanuni inamruhusu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani kuteua wajumbe 4 kuungana na wajumbe wengine kuunda kamati ya Fedha na Mipango baada ya uteuzi huo kuridhiwa na Baraza la Madiwani.Kupitia kanuni hiyo,Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani, Mheshimiwa Bahati Henerico ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Rwabwere aliwateua Mheshimiwa Fredrick Bishanga  (Diwani kata ya Bugara), Mheshimiwa Aloyce Mwinyi  (Diwani kata ya Isingiro),Mheshimiwa Yasinta Katita  (Diwani Viti Maalum), na Mheshimiwa Devotha Biashara  (Diwani Viti Maalum) kuwa wajumbe wa Kamati ya Fedha.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI KADA YA AFYA July 09, 2024
  • TANGAZO LA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA UTOAJI WA VITAMINI A NA UPIMAJI WA HALI YA LISHE KWA WATOTO WA UMRI KUANZIA MIEZI 6 HADI 59 November 27, 2023
  • TANGAZO LA MABADILIKO YA BEI YA USHURU WA MKUNGU WA NDIZI December 31, 2023
  • Tazama vyote

Habari mpya

  • MNASTAHILI PONGEZI KWA USIMAMIZI, UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 07, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA KYERWA

    April 29, 2025
  • TUNAPASWA KUULINDA MUUNGANO WETU-DC. MSOFE

    April 26, 2025
  • ‘TAULO HIZI ZITAWASAIDIA WATOTO KUSOMA KWA UHURU NA UTULIVU’

    March 07, 2025
  • Tazama vyote

Video

Kamati ya siasa ukaguzi wa Miradi Kyerwa
Video zaidi

Viungio

  • Dira na dhima ya Halmashauri
  • Maktaba ya picha

Viungio linganishi

  • Tovuti ya Mkoa wa Kagera
  • Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa
  • Salary Slip
  • Ofisi ya Rais, TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Ikulu

Kifuatilia wageni

world map hits counter

Mapokezi ya wageni

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    Kyerwa District Council

    Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA

    Simu ya mezani: +255 686 397 972

    Simu ya Mkononi: +255 754 422 746

    Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved