Shirika la Kilimo na Chakula Duniani, FAO limeendelea kufadhili Wilaya ya Kyerwa. Hivi karibuni Shirika baada ya kuombwa limesaidia mashine matenki ya maji kwa ajili ya shughuli za umwagiliaji wa bustani za mbogamboga na matunda. hii ni kwa ajili ya kuhakikisha lishe ngazi ya kaya inaimarika na kipato kinaongezeka. Wameombwa na kuamua kufadhili vifaa hivyo vya umwagiliaji kwa ajili ya kuhakikisha chakula kinapatikana kwa kaya zitakazonuafaika na kipato kinaongezeka kwa mwaka mzima bila kujali majira ya mwaka na mabadiliko ya tabia ya nchi. Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kupitia Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wake imeshukuru kupatikana kwa vifaa hivyo kwakuwa vitachangia kuboresha afya ya wananchi na kupunguza ulemavu wilayani Kyerwa. Aidha Shirika limeombwa kuendele kufadhili pale linapoweza ili kuendelea kuboresha afya na lishe kwa wananchi na limeahidiwa kupewa ushirikiano wa kutosha na Serikali.Kabla ya kupatiwa vifaa hivyo vikundi vya vijana vilipewa elimu na mafunzo juu ya ujasiliamali, hivyo wameaswa watumie elimu hiyo ili waweze kunufaika kutokana na kilimo hicho cha bustani.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved