Hayo yamesemwa na Mheshimiwa Kanali Mstaafu Shaban I. Lissu wakati wa kikao cha Baraza la madiwani maalum kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2017.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Kyerwa tarehe 20 Julai,2017,Mkuu wa Wilaya Shaban Lissu (ambaye alimuwakilisha Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera kama Mgeni Rasmi) alisisitiza watumishi kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kwa kutokuzingatia taratibu ili kuepuka hoja zisizo za lazima.
Aidha, Mheshimiwa Kashunju Runyogote ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri aliwashukuru Madiwani kwa kuisimamia vizuri Menejimenti ya Halmashauri mpaka kupata hati safi ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Katika kutoa ushauri kwa Baraza la Madiwani, ndugu Amosi Siabo ambaye ni Kaimu Mkaguzi wa n’nje Mkoa wa Kagera, alisisitiza watendaji wa Halmashauri badala ya kujibu hoja zinazoibuliwa na wakaguzi, ni vema wadhibiti vyanzo vinavyosababisha hoja hizo kuibuliwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved