Katika kuelekea miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Tar. 22, Aprili 2024 katika Wilaya ya Kyerwa imefanyika Dua Maalumu ya kuliombea taifa ambayo imefanyika katika viwanja vya Isingiro Stesheni katika Kata ya Isingiro.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Dua hiyo amesema Watanzania na Wanakyerwa wanatakiwa kuudumisha muungano wa Tanganyika na Zanzabar huku akiwataka viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa kila siku na sio kuishia katika viwanja hivyo.
Dua hiyo iliongozwa na viongozi wa Dini iliambatana na zoezi la uzinduzi wa chajo dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kwa watoto wa kike wenye umri wa kuanzia miaka tisa hadi kumi na nne ambayo itaendelea hadi tar 26 Aprili mwaka huu.
Vile vile kulikuwa na michezo mbalimbali ambayo ilihusisha timu za watumishi wa umma na wananchi wa Wilaya ya Kyerwa.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru inasema, “miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa Letu”.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved