Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu, Dkt. Charles Msonde leo tarehe 1 Juni 2024 amekutana na kufanya kikao na walimu wote wa shule za msingi na sekondani katika Wilaya ya Kyerwa.
Akizungumza na walimu, Dkt. Msonde ameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabali walimu ikiwa ni pamoja na kutokupanda madaraja kwa wakati, kuhamishwa vituo vya kazi bila kulipwa stahiki zao, madai ya fedha za likizo na malimbikizo ya mishahara. Aidha alitolea ufafanuzi wa juhudi za Serikali katika kutatua changamoto.
Dkt. Msonde amesema mwaka huu katika Wilaya ya Kyerwa, jumla ya walimu 1,434 watapandishwa madaraja ambapo 526 watapanda kwa mserereko na 908 watapanda kawaida huku wenye malimbikizo ya mishahara na madeni mbalimbali yatashughulikiwa haraka kwa utaratibu mzuri uliowekwa na serikali.
Pia amewataka walimu kufundisha kwa bidii, maarifa na kuwa wabunifu katika kazi zao ili kuboresha elimu ya wanafunzi na kufikia dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha Sekta ya Elimu.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved