Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa SACF. James John akiambatana na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri, leo tarehe 10 Julai 2023 wametembelea miradi ya maendeleo na maeneo pendekezwa yatakayopitiwa na mwenge wa uhuru mwaka 2023.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi amejionea maendeleo ya miradi hiyo na kutoa maagizo kwa wasimamizi wa miradi kwa kuwataka wakamilishe taratibu, nyaraka na vitu vyote vinahitajika kwa hizi siku chache zilizobaki kabla ya ujio wa mwenge.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na madarasa matano ya Shule ya Sekondari Nkwenda na kujionea uchongoji wa samani za, viti 80, madawati 80, pamoja na viti vitano na meza tano za waalimu ambavyo vitatumiwa na wanafunzi na waalimu wa Shule ya Sekondari Nkwenda. Eneo la upandaji miti 500 katika shule ya msingi Kaaro, jengo la wodi ya wanaume wa magonjwa mchanganyiko katika Kituo cha Afya Nkwenda na viwanja vya stendi ya mabasi Kwenda ambavyo vitatumika katika sherehe za mkesha wa mwenge wa uhuru.
Miradi mingine ni kisima cha maji cha Kagenyi-Omukalinzi, kiwanda cha kukoboa kahawa cha Chama cha Ushirika cha Msingi Mkombozi pamoja na kutembele kipande cha barabara ya lami yenye urefu wa km 1.2 eneo la Rwenkorongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Mwenge wa uhuru unatarajiwa kuanza mbio zake tar. 8 Agasti katika mkoa wa Kagera na katika Wilaya ya Kyerwa ni tar. 12 Agasti mwaka huu, ambapo miradi mbalimbali itatembelewa na kuwekewa jiwe la msingu huku mingine ikuzinduliwa na kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni; Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved